Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Refrain

Tanzania nakupenda nchi yangu nakupenda sana

Bara pia visiwani sisi sote tupendane sana

1. Tanzania yetu twakupenda kwa hakika

Uumbaji wake Mungu wetu ndio twausifu milele

Bahari zake alizotupa ndizo twajivunie leo

Bahari zake alizotupa ndizo twajivunie leo

2. Maziwa na vito nazo mbuga za wanyama

Mlima mrefu Kilimanjaro upitao yote Afrika

Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni

Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni

3. Taifa la amani na upendo kwa hao wote

Dumisha umoja Mungu Baba, na utuepushe na vita

Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja

Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja

Acacia Singers, Tz.

Comments

Popular posts from this blog

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA