Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania
Refrain
Tanzania nakupenda nchi yangu nakupenda sana
Bara pia visiwani sisi sote tupendane sana
1. Tanzania yetu twakupenda kwa hakika
Uumbaji wake Mungu wetu ndio twausifu milele
Bahari zake alizotupa ndizo twajivunia leo
Bahari zake alizotupa ndizo twajivunia leo
2. Maziwa na vito nazo mbuga za wanyama
Mlima mrefu Kilimanjaro upitao yote Afrika
Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni
Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni
3. Taifa la amani na upendo kwa hao wote
Dumisha umoja Mungu Baba, na utuepushe na vita
Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja
Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja
Acacia Singers, Tz.