Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers
Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers
1. Ninakushukuru kwa wema wako
Mungu mtukufu wa kuabudiwa
Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine
Umenishindia yaliyo makuu
Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine
Umenishindia yaliyo makuu
Refrain
Ni wewe tu Bwana Mungu wangu
Wala hakuna yeyote kama wewe
Ni wewe tu Bwana Mungu wangu
Ndiwe mfariji wangu hakuna mwingine
2. Uweza na nguvu (Yote) na mamlaka
Yashinda wakuu wote wa dunia
Nionapo milima, jua, mwezi na nyota
Wewe ni mkuu haulinganishwi
Nionapo milima, jua, mwezi na nyota
Wewe ni mkuu haulinganishwi
3. Nikifika kwako huko mbinguni
Nitakusujudu we mtakatifu
Sifa na heshima viwe nawe milele
Watu maelufu kukusujudia
Sifa na heshima viwe nawe milele
Watu maelufu kukusujudia.
Acacia Singers, Tz.
Comments
Post a Comment