Thursday, 30 October 2025

Nenda Ninawi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nenda Ninawi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


Verse 1

Nenda Ninawi,

Peleka ujumbe (peleka ujumbe)

Peleka ujumbe (peleka ujumbe)

Nenda Ninawi Yona, Peleka ujumbe wangu

Kwamba uovu wao umefika mbele yangu


Verse 2

Kawaambie watubu (Kawaambie watubu)

Nitangaamiza Ninawi (Nitangaamiza Ninawi)

Kaipaze sauti (Kaipaze sauti)

Watu wote wanapaswa kutubu,

Wanadamu na wanyama

Na vyote vilivyoumbwa na Mungu,

Vyote vimlilie Mungu muumbaji


Verse 3

Yona hakutaka kwenda Ninawi

Kapanda merikebu ya Tarshishi

Akijua anamkimbia Mungu

Masikini Yona mtumishi wa Mungu hakujua,

Mungu yuko pande zote


Verse 4

Wakiwa baharini tufani ikavuma

Upepo ukaipiga ile merikebu

Meli ikatikiswa (ikatikiswa)

Karibu ya kupasuka vipande vipande (vipande vipande)

Yona hana habari (hana habari)

Amefichiwa na usingizi (usingizi)

‘Amka! Wewe, Amka! Wewe,

Usilale usingizi,

Muombe Mungu wako atuokoe’


Verse 5

Yona alipoamka na kuona tufani,

Akagundua kosa lake kwa Mungu

Kamwambia nahodha,

‘Ili ninyi mpone…,

Nitupeeni mimi baharini’


Verse 6

Mimi na wewe rafiki,

Tumetumwa mara ngapi na Mungu?

Hatupeleki ujumbe tuliotumwa na Baba

Kwa ujinga tunadhani twajificha

Hebu leo tuwe kama Yona

Tugeuke na kwenda kufanya kazi

Bwana anatutuma…


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 35, Kurasini Acapella, Bedi Score, Bedi Lyrics

Sunday, 19 October 2025

Upendo wa Yesu Lyrics sung by Light Group Ministry

Upendo wa Yesu Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Upendo wa Yesu kwangu

Upendo usiokipimo

Japo dunia iishe ndugu

Upendo wa Yesu waninitosha


Chorus

Upendo wa Yesu kwangu watosha

Hakuna cha kulinganishwa na dunia hii

Nimetafuta kote

Hakuna upendo mwingine kama wa Yesu


2. Upendo ulimfanya

Muumba wa mbingu na nchi

Ashuke chini kutufilia

Kutuokoa kwa dhambi zetu


3. Aliuwawa Bwana Yesu

Kifo hicho cha msalaba

Upendo wake kwa wenye dhambi

Ulimpa kifo cha aibu.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics

Sikia Sauti Ya Bwana Lyrics sung by Light Group Ministry

Sikia Sauti Ya Bwana Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Sikia sauti ya Bwana Inenayo moyoni

Subira inanijia Kwa maneno hayo

Giza litatoweka Majaribu yakome

Subiri nuru ijayo Mvua itapokoma


Chorus

Manemo matamu Yanayonipa nguvu

Yanituliza moyo Nipitapo shidani


2. Hata katika dhiki Nipitapo bondeni

Hatari zinikumbapo Yeye huniongoza

Huzuni zinikumbapo Kamwe sitachoka

Subiri nuru ijayo Mvua itakapokoma.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Whispering Hope/Soft as the Voice of an Angel

Panapo Pendo Lyrics sung by Light Group Ministry

Panapo Pendo Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Vitu vyote ni sawa, Panapo pendo

Kila sauti tamu, Panapo pendo

Pana amani pale, Na furaha nyumbani

Siku zote salama, Panapo pendo


Chorus

Panapo upendo,

Siku zote salama,

Panapo pendo.


2. Furaha i nyumbani, Panapo pendo

Hapana machukizo, Panapo pendo

Chakula ni kitamu, Mashamba ya sitawi

Maisha ni kamili, Panapo pendo


3. Hata mbinguni juu, Pana furaha

Wakiona upendo, Nyumbani mwetu

Macho yanapendezwa, Na viumbe vya Mungu

Naye Mungu huona, Panapo pendo


4. Ee Yesu niwe wako, Wako kabisa

Ndipo patakuwako, Pendo nyumbani

Nitakaa salama, Sitaifanya dhambi

Nitabarikiwa tu, Panapo pendo.


From: Nyimbo za Kristo No 184.

Writer: John Hugh McNaughton.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics

Pana Mahali Pazuri Mno Lyrics sung by Light Group Ministry

Pana Mahali Pazuri Mno Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Pana mahali pazuri mno

Twapaona kwa mbali sasa

Baba yetu angoja pale

Amepanga makao yetu


Refrain

Kitambo tu bado

Tutakutana ng’ambo pale

Kitambo tu bado

Tutakutana ng’ambo pale


2. Tutaimba pale kwa moyo

Nyimbo tamu za wenye heri

Na rohoni hatutaona

Tena haja ya kupumzika


3. Kwa Baba yetu mkarimu

Tutatoa shukrani sana

Kwa kipaji cha pendo lake

Na baraka anazotupa.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Nyimbo za Kristo No. 180 (In the Sweet By and By/There’s a Land)

Nipe Neno Lyrics sung by Light Group Ministry

Nipe Neno Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Nipe neno niweze kusema

Itakayo mbingu kwa wanadamu

Walioasi warejeshwe zizini mwako


Chorus 

Umetupa mamlaka duniani kote

Tulihubiri neno lako

Tukawaletee walopotea

Warejee kwako


2. Kwa imani kamwe sihofu

Neno lako faraja kwa waloasi

Wasikiapo warejee zizini mwako.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics

Niimbe Pendo Lake Lyrics sung by Light Group Ministry

Niimbe Pendo Lake Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Niimbe (Niimbe) pendo lake,

Pendo la (Pendo la) Yesu Bwana;

Sababu (Sababu) alitoka

Kwa Baba, akafa


Chorus

Niimbe (Niimbe) pendo lake;

Sifa kuu (Sifa kuu) nitatoa;

Akafa (Akafa) niwe hai,

Niimbe pendo lake


2. Machozi (Machozi) alitoa 

Ijapo (Ijapo) sijalia;

Maombi (Aaombi) yangu bado,

Aniombeapo


3. Upendo (Upendo) kubwa huo!

Dunia (Dunia) haijui

Samaha (Samaha) kwa makosa

Kubwa kama yangu


4. Hapana (Hapana) tendo jema

Ambalo (Ambalo) nilitenda,

Nataka (Nataka) toka leo 

Nimwonyeshe pendo.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Nyimbo za Kristo No. 031 (I Will Sing of Jesus Love)

Ni Yeye Lyrics sung by Light Group Ministry

Ni Yeye Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Ni yeye anayejua shida zetu,

Kwani ndiye aliyetufilia

Aliacha enzi yake kule juu,

Wewe nami tuokolewe


Refrain

Ndiye Yesu Mwokozi

Anatutakasa 

Ajua shida zetu

Nani kama yeye?


2. Ni yeye anayejua shida zetu,

Majaribu tunayoyapitia

Hata pale tunapokata tamaa

Bado yu mwaminifu kwetu.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics

Mlangoni Pa Moyo Lyrics sung by Light Group Ministry

Mlangoni Pa Moyo Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Mlangoni pa moyo; Mgeni! (Amesimama)

Amesimama pale, Mgeni! (Amesimama)

Umkaribishe sasa,

Umkaribishe Mwana

Wa Baba wa upendo: Mgeni! (Umkaribishe)


2. Moyo wako kwa Bwana, Fungua (Fungulieni)

Asikuache mbali, Fungua (Fungulieni)

Umkubali Rafiki,

Roho atafariji

Naye atakutunza: Fungua (Fungulieni) 


3. Usikie sauti Ya Bwana (Uisikie)

Uyachague mambo Ya Bwana (Mambo ya Bwana)

Ufungue mlango,

Usimwambie bado

Jina lake tumai; Yu Bwana (Jina la Bwana)


4. Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)

Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)

Uzuri utavikwa

Dhambi ataondoa,

Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni)


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Nyimbo za Kristo No. 157 (There's a Stranger at the Door)


Ombi Langu Lyrics sung by Light Group Ministry

Ombi Langu Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Mara nyingi nimezama katika mawazo

Hata lini shida za dunia zitakoma

Lakini najua siku itafika

Haya yote yatapita Siku ile Yesu arudipo


Refrain

Majina yaitwapo Jina langu na liwepo

Watakatifu wasimamapo Nami niwe kati yao

Wakivikwa taji (Taji yangu mimi nayo) Taji yangu na iwepo

Ombi langu Bwana (Ewe Yesu) Nikuone katika utukufu wako

Ombi langu Bwana (Ewe Yesu) Nikuone katika utukufu wako


2. Wengi wameacha nuru iliyo ya kweli

Wamezamia mambo ya dunia yapitayo 

Lakini najua siku itafika 

Haya yote yatapita siku ile Yesu arudipo.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ikumbukeni Sabato Lyrics sung by Light Group Ministry

Ikumbukeni Sabato Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Ikumbukeni Sabato Sabato ya Bwana

Siku nzuri yenye raha Kupita siku zote

Siku nzuri yenye raha Kupita siku zote


Chorus

Ni mpango wa Mungu Kwa kupanga siku sita

Kutana siku ya saba Sabato takatifu

Kutana siku ya saba Sabato takatifu


2. Moyo wangu wanivuta Niingie Sabato

Ili kujifurahisha Kwa mambo ya Mungu.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Adapted from Nyimbo za Kristo No. 084 (Don’t Forget the Sabbath

Hatujui Saa Lyrics sung by Light Group Ministry

Hatujui Saa Lyrics sung by Light Group Ministry


1. Hatujui saa ya kuja kwwa Bwana,

Lakini dalili zasema karibu

Atakaporudi, lakini kwa kweli

Hatujui saa


Chorus

Atakuja, kwa vile tukeshe;

Atakuja Mwokozi, Aleluya!

Atakuja kwa fahari ya Baba yake,

Hatujui saa


2. Pana nuru kwao wapendao haki,

Pana kweli katika chuo cha Mungu;

Unabii hufundisha kuja kwake,

Hatujui saa


3. Tutakesha na tutaomba daima,

Tutafanya kazi mpaka akija,

Tutaimba na tutasoma ishara,

Hatujui saa.


Light Group Ministry.


Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics


Nyimbo za Kristo No. 173 (We Know Not the Hour)

Sunday, 12 October 2025

Tutaingia Mji Lyrics sung by Hope Voice Group

Tutaingia Mji Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Tutaingia mji mtakatifu, Yerusalemi mji wa Mungu

Washindi wote tutaingia, Tutalakiwa na Bwana wetu Yesu

Washindi wote tutaingia, Tutalakiwa na Bwana wetu Yesu


Refrain

Tutakusanyika mbele zake, Mungu wetu

Mataifa yote, lugha hata na jamaa

Tutashangilia wokovu wetu milele na milele


2. Mwokozi wetu atatukaribisha, Tutashangaa kwa mambo mapya

Tutaonana na ndugu zetu, Tulotengana sababu ya mauti

Tutaonana na ndugu zetu, Tulotengana sababu ya mauti


3. Mji wa Mungu ni mji wa amani, Hakuna vita wala mauti

Tupige vita tushinde wote, Na tuingie tuishi naye Bwana

Tupige vita tushinde wote, Na tuingie tuishi naye Bwana.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Tule Nini Lyrics sung by Hope Voice Group

Tule Nini Lyrics sung by Hope Voice Group


1 ‘Tule nini? Tuvae nini?’ Tumwachie Bwana


Tunahangaika usiku na mchana

Kwamba tule nini, Tuvae nini

Hata twamsahau Bwana

Hapa duniani sote tuwapitaji

Hata muda wetu ni mfupi

Twapita kama maua


Refrain

Bwana asema, ‘Tazameni ndege wa angani

Hata maua ya kondeni yanavyochanua

Nyinyi je si bora, kuliko wao?

Tafuteni ufalme wa Mungu wetu

Nayo, Mahitaji mtazidishiwa’


2. Kwa kuhangaika twadhani twaongeza

Hata kimo chetu, Maisha yetu

Pasipo na Bwana Mungu,

Tunajidanganya tunapotegemea

Hasa nguvu zetu akili zetu,

Na kumsahau Bwana.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Tafakari Upendo Lyrics sung by Hope Voice Group

Tafakari Upendo Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Tafakari upendo wa Yesu, Kwa wanadamu wote

Aliacha enzi utukufu wake, Kazaliwa horini mwa wanyama

Aliacha enzi utukufu wake, Kazaliwa horini mwa wanyama


Refrain

Anabisha mlangoni, Anataka kuingia

Mruhusu aingie, Afanye makao nawe

Ooh - Fungua mlango Yesu aingie, Uwe ni kiumbe kipya

Ooh - Fungua mlango Yesu aingie, Uwe ni kiumbe kipya


2. Kuja kwake kuzaliwa kwake, Dhihirisho la pendo

Aliacha yote kwa ajili yako, Mfalme kazaliwa kwa aibu

Aliacha yote kwa ajili yako, Mfalme kazaliwa kwa aibu


3. Mruhusu azaliwe kwako, Ndani ya moyo wako

Atabadilisha yaliyo magumu, Nawe utakuwa kiumbe kipya

Atabadilisha yaliyo magumu, Nawe utakuwa kiumbe kipya.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Pumzi Ya Uhai Lyrics sung by Hope Voice Group

Pumzi Ya Uhai Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Pumzi ya uhai inapotoweka, Mwili ukibaki pekee yake

Pale pale tukiwa tumelala, Neno lasema tumekufa

Pale pale tukiwa tumelala, Neno lasema tumekufa


Refrain

(Kifo) Kifo umetutenga na wazazi,

Umetutenga na watoto wetu

Wapendwa wengi wamelala,

Wanasubiri ufufuo


2. Mwili ukishushwa ndani ya kaburi, Watu wakilia kwa huzuni

Matumaini yao yatoweka, Wengi hawana msaada

Matumaini yao yatoweka, Wengi hawana msaada


3. Tunaye rafiki aloshinda kifo, Aliyefufuka toka kwa wafu

Ndiye Yesu Mwokozi wa dunia, Tukimwamini tutaishi

Ndiye Yesu Mwokozi wa dunia, Tukimwamini tutaishi.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Parapanda Ya Bwana Lyrics sung by Hope Voice Group

Parapanda Ya Bwana Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Parapanda ya Bwana italia,

Wafu wote watafufuka (Watafufuka)

Ni wale tu waliotunza agano,

Kati yao na Mungu wao


Refrain 1

Watashangilia kushinda kifo,

Wataruka (ruka ruka) kama ndama

Wataishi naye Mwokozi wao,

Siku zote (milele) hata milele


2. Siku hiyo machozi yatakoma,

Watu wote washangilia (Washangilia)

Tutasema u wapi ewe mauti,

Chanzo chako kushinda kwako?


(Refrain 1)


3. Kamwe hatutaweza tangulia-aah,

Kumlaki Bwana ajapo (Bwana ajapo)

Walolala watafufuliwa kwanza,

Kwa pamoja tutamlaki.


Refrain 2

Tutashangilia kushinda kifo,

Tutaruka (ruka ruka) kama ndama

Tutaishi naye Mwokozi wetu,

Siku zote (milele) hata milele.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ondoka Ukatangaze Lyrics sung by Hope Voice Group

Ondoka Ukatangaze Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Ondoka ukatangaze hukumu (Ya Bwana), Mwisho umekaribia watubu

Waeleze kwamba Bwana yuaja, Kuhukumu watu wote kwa haki

Watangazie kwamba mwisho uko karibu, Watasimama mbele ya kiti cha hukumu

Watangazie kwamba mwisho uko karibu, Watasimama mbele ya kiti cha hukumu


Refrain

Ondoka, Peleka neno kwa wahitaji, Huduma yako yahitajika

Ni agizo lake Mungu wetu, Watu waokolewe


2. Tazama mavuno yamekomaa, Nani kwenu yu tayari aende

Ni agizo lake Bwana kwa wote, Waitwao wanafunzi wa kweli

Watasimama kuwaonya watu watubu, Wawe tayari kwa siku ile ya hukumu.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Tafakari (Itakuwaje) Lyrics sung by Hope Voice Group

Tafakari (Itakuwaje) Lyrics sung by Hope Voice Group


Prelude

Uuuh-Uuuuh, Uuuh-Uuuuh

Uuuh-Uuuuh, Uuuh-Uuuuh


Tafakari,


1. Hebu tafakari kisa kile cha wakati wa Nuhu

Waliangamizwa watu wengi kwani hawakujali


Refrain 1

Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa

Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa


Itakuwaje siku ile ya mwisho?

Tutaponaje?

Tusipojali wokovu tutaponaje siku hiyo?


Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa

Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa


2. Hata katika siku za Lutu walikataa onyo

Waliangamizwa watu wengi kwani hawakujali


Refrain 1


3. Ni mara ngapi rafiki yangu umekataa onyo?

Ni mara ngapi rafiki yangu umepuuza wito?


Refrain-2

Sasa utaponaje ndugu kama usipojali?

Utakuwa sawa na wale walioangamizwa

Sasa utaponaje ndugu kama usipojali?

Utakuwa sawa na wale walioangamizwa


Itakuwaje siku ile ya mwisho?

Tutaponaje?

Tusipojali wokovu tutaponaje siku hiyo?


Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa

Sasa tutaponaje sisi kama tusipojali?

Tutakuwa sawa na wale walioangamizwa.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Machoni Pa Bwana (Mtini Kalvari) Lyrics sung by Hope Voice Group

Machoni Pa Bwana (Mtini Kalvari) Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Machoni pa Bwana sote tu wenye dhambi

Ajabu pendo lake Ni pendo lililo kuu


Lililotutafuta ingawa tulikosa

Ni pendo la ajabu Yesu alionyesha

Lililotutafuta ingawa tulikosa

Ni pendo la ajabu Yesu alionyesha


Refrain

Mtini (Mtini) Kalvari

Yesu alionyesha upendo wake kweli,

Kila amwaminiye yu na uzima tele


Mtini (Mtini) Kalvari

Yesu alishalipa madai ya Shetani

Kila amwaminiye yu na uzima tele


2. Japo tulikosa tukamuasi Mungu

Alimtuma Mwana mpatanishi wetu


Ni kwa neema yake sote twaokolewa

Ni pendo la ajabu Bwana alionyesha

Ni kwa neema yake sote twaokolewa

Ni pendo la ajabu Bwana alionyesha.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Msifadhaike Mioyoni Lyrics sung by Hope Voice Group

Msifadhaike Mioyoni Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Msifadhaike mioyoni mwenu

Mnawamini Mungu Baba niamini nami

Nyumba mwa Baba kuna makao mengi

Kama si hivyo ningaliwaambia

Nyumba mwa Baba kuna makao mengi

Kama si hivyo ningaliwaambia


Refrain

Bwana wetu uje sasa mioyo yakusubiri

Mapambazuko yakaribia (Yakaribia)

Si mbali mbali yuaja, Bwana wa utukufu

Kuwachukua wateule wake

Si mbali mbali yuaja, Bwana wa utukufu

Kuwachukua wateule wake


2. Miaka imepita siku zaenda

Mwokozi wetu uje sasa tunakusubiri

Tunahangaika nayo maisha haya

Uje Mwokozi tunakusubiri

Tunahangaika nayo maisha haya

Uje Mwokozi tunakusubiri.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

Mapambazuko Lyrics sung by Hope Voice Group

Mapambazuko Lyrics sung by Hope Voice Group


1. Mapambazuko yako karibu Tuweni macho na ya dunia

Mapambazuko yako karibu Tuweni macho na ya dunia

Tuyaonayo yanaonyesha Mwokozi wetu yu mlangoni


Refrain

(Naacha) Naacha ya dunia nakwenda kwa Yesu

Sihitaji chochote nataka nimwone Bwana


Dunia sio kwetu (Kwetu), Kwetu ni juu mbinguni

Hitaji la moyoni (yoni) umpokee Yesu wangu

Dunia sio kwetu (Kwetu), Kwetu ni juu mbinguni

Hitaji la moyoni (yoni) umpokee Yesu wangu


2. Mwisho wa yote Tutapumzika Taabu zote zitatoweka

Mwisho wa yote Tutapumzika Taabu zote zitatoweka

Mwokozi Yesu Atayafuta machozi yote Kwa watu wake.


Hope Voice Group.


Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics

There’s a Time Lyrics sung by Saro's Family

There’s a Time Lyrics sung by Saro's Family


Verse 1

There’s a time you feel lonely

A time you are so weary

And you look around

You hope to find somebody

But nobody cares for you

So you look for direction,

‘Cause you have no peace in you

Just turn your eyes on him

He is more than ready,

To lift you up (To lift you, to lift you up)


Verse 2

Remember the promise that Jesus promised

To be with you till the end

And he will send His Holy Spirit

To teach and guide you

So don't you worry, And never give up

The Lord is with you All the way, everyday

The Lord is with you All the way, everyday


Verse 3

So come ma’ Lord

Come rescue me

I say come my Lord

Come rescue me

I can never make it alone


Verse 4

Alone I can’t (cannot)

Alone I won’t (will not)

Alone I can’t (cannot)

Alone I won’t (will not)

Alone I can’t (cannot)

Alone I won’t (won’t)


Verse 4b Outro

I can never make it alone.

I can never make it alone.


Saro's Family.


Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics

Njooni Tusemezane Lyrics sung by Saro's Family

Njooni Tusemezane Lyrics sung by Saro's Family


Chorus

“Njooni tusemezane,” Asema Bwana, “Dhambi zenu...

“Njooni tusemezane,” Asema Bwana,


“Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitakuwa nyeupe,

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitasafirishwa kabisa


Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitakuwa nyeupe,

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitasafirishwa kabisa”


Verse 1

Kwa jinsi hii hii ya upendo mkubwa

Mungu alimtoa mwanawe pekee

Akafa msalabani, Kwa sababu ya dhambi zetu


Chorus

“Njooni tusemezane,” Asema Bwana, “Dhambi zenu...

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitakuwa nyeupe,

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitasafirishwa kabisa”


Verse

Tubuni dhambi, Na mkarejee

Mshahara wa dhambi, Ni mauti jameni

Ni dhambi zilizofanya, Bwana Yesu asulubiwe


Chorus

“Njooni tusemezane,” Asema Bwana, “Dhambi zenu...

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitakuwa nyeupe,

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitasafirishwa kabisa


Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitakuwa nyeupe,

Dhambi zenu, Japo nyekundu, Zitasafirishwa kabisa”


Saro's Family.


Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics

Nasema Njoo Ndani Yangu Lyrics sung by Saro's Family

Nasema Njoo Ndani Yangu Lyrics sung by Saro's Family


Verse I

Ooh,

Nasema Njoo, Ndani yangu 

                        (Nasema njoo)

Ndani ya moyo wangu (Ndani yangu)


Nasema Njoo, Ndani yangu 

                       (Nasema njoo)

Ndani ya moyo wangu (Ndani yangu)

Moyo wangu chunguza (Ewe Baba)

Macho yangu tawala, Bwana

Macho yangu tawala, Bwana


Verse II

Tawala mwili wangu; Ni hekalu (Wangu)

Ukiwa ndani yangu; Nina uzima tele

Tawala moyo wangu (Moyo); Ni chemichemi (Chemichemi)

Ukiwa ndani yangu; Nina uzima tele


Verse IIIa

Nimechoka (Nimechoka) Nime…(Baba) Nimechoka (Nimechoka)

Kutawalwa na yule mwovu Shetani, Baba

(Ooh Niokoe) Niokoe, (Niokoe) Niokoe (Niokoe)

Nimezama dhambini ninapotea, Baba

Nisamehe (Nisamehe), Nisamehe, Ewe Baba

Dhambi zangu ni nyingi zanilemea, Baba

N’shike mkono (‘Shike mkono), N’shike mkono (‘Shike mkono)

Kutembea upweke mimi nashindwa, Baba

(Unishindie) Unishindie, Unishindie (Nishindie) (Ewe Baba)

Nguvu zake Shetani zanilemea Baba


Verse IIIb (Outro)

Nimechoka, Nimechoka, Ewe Baba

Kutawalwa na yule mwovu Shetani, Baba


(Uniokoe) Niokoe, Niokoe (Uniokoe)

Nimezama dhambini ninapotea, Baba

Nisamehe (Nisamehe), Nisamehe (Baba)

Dhambi zangu ni nyingi zanilemea Baba

N’shike mkono (‘Shike mkono), N’shike mkono (‘Shike mkono)

Kutembea upweke mimi nashindwa Baba…


Saro's Family.


Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics

I Have Found Lyrics sung by Saro's Family

I Have Found Lyrics sung by Saro's Family


Verse

I have...

I have…

I have found somebody ah, Somebody (Somebody)

I have found somebody ah, Somebody (Somebody)

I have found somebody who cares for me (for me)


And I know who-Uuh…

And I know who-Uuh…

And I know there's nothing to worry (To worry)

I know you may not agree

And I know you may not believe me

I know you may not agree

And I know you may not believe me


Refrain

I/Uh have… (I have found) 

O yes, I have; Jesus Christ

Jesus; He’s more than golden money

Uuh/+However, (However),

Oh yes, However, Sophisticated

However, A weapon will not kill my soul


Down he came, Uuh

And died for me, Uuh

Nothing more I need from him than eternal life

Down he came, Uuh

And died for me Uuh

Nothing more I need from him than eternal life


Verse

He doesn't…

He doesn't…

He doesn't count anybody’s sins (Sins)

He doesn't count anybody’s sins (Sins)

He doesn't count anybody’s sins (Sins)

If you repent Uuh…

If you repent Uuh…

If you repent from deep in your heart (In your heart)

And like the law which is harsh-?

And like the law which is harsh

And like the law which is harsh

And like the law which is harsh


Refrain

I have… (I have found) 

O yes, I have; Jesus Christ

Jesus; He’s more than golden money

However, (However)

Oh yes, However, Sophisticated

However, A weapon will not kill my soul


Down he came, Uuh

And died for me Uuh

Nothing more I need from him than eternal life

Down he came, Uuh

And died for me Uuh

Nothing more I need from him than eternal life


I have… (I have found) 

O yes, I have; Jesus Christ

Jesus; He’s more than golden money

However, (However)

Oh yes, However, Sophisticated

However, A weapon will not kill my soul


Outro

However, (However)

Oh yes However,

Sophisticated!


Saro's Family.


Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics


And like the law which is harsh-?; The law of God is harsh. No linear word sounds the same as harsh in above lines.

Fungana Virago Lyrics sung by Saro's Family


Rrelude
Ah, We, Toka,
Ah, Shetani, Nenda, Ah
Toka! Toka! Toka!

Chorus 1
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako (Shetani wee)
Fungana fungana virago (Wewe)
Shika njia nenda zako wee
Fungana fungana virago (Shetani)
Shika njia nenda zako (Ebu we)
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee

Verse 1/Chorus 2
Umenitosha Umen'sumbua
Shika njia nenda zako wee
Umenichosha Wanikanganya
Shika njia nenda zako
Wala sio nyumba yako, Shetani

Chorus 1
Fungana fungana virago (Toka)
Shika njia nenda zako (Nenda)
Fungana fungana virago (Toka)
Shika njia nenda zako wee (Toka Toka wee)
Fungana fungana virago (Nenda)
Shika njia nenda zako (Toka)
Fungana fungana virago (Toka)
Shika njia nenda zako wee (Toka Toka wee)

Verse 2
Wacha niseme wala hakuna utani
Ikiwa Shetani ndiye dereva jamani
Basi samahani maovu yote ni ndani
Basi samahani maovu yote ni ndani

Verse 1/Chorus 2
Umenitosha Umen'sumbua
Shika njia nenda zako wee
Umenichosha Wanikanganya
Shika njia nenda zako
Mwili wangu ni hekalu wee
Wala sio nyumba yako, Shetani

Chorus 1
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee

Verse 3
Nimejitoa leo najaa nipokee
Haya najaa nipokee
Nasema nakuja leo Bwana nipokee
Haya najaa nipokee

Verse 1/Chorus 2
Umenitosha Umen'sumbua
Shika njia nenda zako wee
Umenichosha Wanikanganya
Shika njia nenda zako
Mwili wangu ni hekalu wee
Wala sio nyumba yako, Shetani

Chorus 1
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee

Verse/Outro Verse
Ah, Shetani jamani amenikamata kooni-? (aah, aah)
Nimekuwa mtumwa, Moyo wangu waumwa (aah, aah)
Ah, Bwana Nishike, Niokoe (aah, aah)
Nishike niokoe (aah, aah)
Nishike niokoe (aah, aah)
Nishike niokoe (aah, aah)

Chorus 1
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako (Nenda zako)
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee (Nenda zako)
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako (Nenda zako)
Fungana fungana virago
Shika njia nenda zako wee (Nenda zako)

Saro's Family.

Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics

Down To Find My Lover Lyrics sung by Saro's Family

Down To Find My Lover Lyrics sung by Saro's Family


Prelude

This goes to all the people;

God so love the world.


1. I’m going down to find my lover

Going down to get my lover

You know,

She lost her way to me;

“Come my bride”

(I’m gonna meet)


Refrain

I say, I better perish for my lover

Oh yes, Hung on the cross for her

Pay the ransom, get my lover

Oh yes, to her my own wife


2. I'm going to that big city (going down)

In that harlotry house

You know, from that lover she has

“Come my bride”

(I'm going down)


Outro

For God so loved the world

He sent Jesus on Earth

Oh Yes, Who hanged on the cross for us

“Come my bride.”

(He so loved the world)


Saro's Family.


*Oh yes, to her my own wife; To get her as my (only) own wife; Presents the ownership Jesus claims on the church as the wife.


Saro’s Family, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...