Parapanda Ya Bwana Lyrics sung by Hope Voice Group
Parapanda Ya Bwana Lyrics sung by Hope Voice Group
1. Parapanda ya Bwana italia,
Wafu wote watafufuka (Watafufuka)
Ni wale tu waliotunza agano,
Kati yao na Mungu wao
Refrain 1
Wataruka (ruka ruka) kama ndama
Wataishi naye Mwokozi wao,
Siku zote (milele) hata milele
2. Siku hiyo machozi yatakoma,
Watu wote washangilia (Washangilia)
Tutasema u wapi ewe mauti,
Chanzo chako kushinda kwako?
(Refrain 1)
3. Kamwe hatutaweza tangulia-aah,
Kumlaki Bwana ajapo (Bwana ajapo)
Kwa pamoja tutamlaki.
Refrain 2
Tutashangilia kushinda kifo,
Tutaruka (ruka ruka) kama ndama
Tutaishi naye Mwokozi wetu,
Siku zote (milele) hata milele.
Hope Voice Group.
Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments