Machoni Pa Bwana (Mtini Kalvari) Lyrics sung by Hope Voice Group
Machoni Pa Bwana (Mtini Kalvari) Lyrics sung by Hope Voice Group
1. Machoni pa Bwana sote tu wenye dhambi
Ajabu pendo lake Ni pendo lililo kuu
Lililotutafuta ingawa tulikosa
Ni pendo la ajabu Yesu alionyesha
Lililotutafuta ingawa tulikosa
Ni pendo la ajabu Yesu alionyesha
Refrain
Mtini (Mtini) Kalvari
Yesu alionyesha upendo wake kweli,
Kila amwaminiye yu na uzima tele
Mtini (Mtini) Kalvari
Yesu alishalipa madai ya Shetani
Kila amwaminiye yu na uzima tele
2. Japo tulikosa tukamuasi Mungu
Alimtuma Mwana mpatanishi wetu
Ni kwa neema yake sote twaokolewa
Ni pendo la ajabu Bwana alionyesha
Ni kwa neema yake sote twaokolewa
Ni pendo la ajabu Bwana alionyesha.
Hope Voice Group.
Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments