Tule Nini Lyrics sung by Hope Voice Group
Tule Nini Lyrics sung by Hope Voice Group
1 ‘Tule nini? Tuvae nini?’ Tumwachie Bwana
Tunahangaika usiku na mchana
Kwamba tule nini, Tuvae nini
Hata twamsahau Bwana
Hapa duniani sote tuwapitaji
Hata muda wetu ni mfupi
Twapita kama maua
Refrain
Bwana asema, ‘Tazameni ndege wa angani
Hata maua ya kondeni yanavyochanua
Nyinyi je si bora, kuliko wao?
Tafuteni ufalme wa Mungu wetu
Nayo, Mahitaji mtazidishiwa’
2. Kwa kuhangaika twadhani twaongeza
Hata kimo chetu, Maisha yetu
Pasipo na Bwana Mungu,
Tunajidanganya tunapotegemea
Hasa nguvu zetu akili zetu,
Na kumsahau Bwana.
Hope Voice Group.
Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments