Nenda Ninawi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Nenda Ninawi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Verse 1
Peleka ujumbe (peleka ujumbe)
Peleka ujumbe (peleka ujumbe)
Nenda Ninawi Yona, Peleka ujumbe wangu
Kwamba uovu wao umefika mbele yangu
Verse 2
Kawaambie watubu (Kawaambie watubu)
Nitangaamiza Ninawi (Nitangaamiza Ninawi)
Kaipaze sauti (Kaipaze sauti)
Watu wote wanapaswa kutubu,
Wanadamu na wanyama
Na vyote vilivyoumbwa na Mungu,
Vyote vimlilie Mungu muumbaji
Verse 3
Yona hakutaka kwenda Ninawi
Akijua anamkimbia Mungu
Masikini Yona mtumishi wa Mungu hakujua,
Mungu yuko pande zote
Verse 4
Wakiwa baharini tufani ikavuma
Upepo ukaipiga ile merikebu
Meli ikatikiswa (ikatikiswa)
Karibu ya kupasuka vipande vipande (vipande vipande)
Yona hana habari (hana habari)
Amefichiwa na usingizi (usingizi)
‘Amka! Wewe, Amka! Wewe,
Usilale usingizi,
Muombe Mungu wako atuokoe’
Verse 5
Yona alipoamka na kuona tufani,
Akagundua kosa lake kwa Mungu
Kamwambia nahodha,
‘Ili ninyi mpone…,
Nitupeeni mimi baharini’
Verse 6
Mimi na wewe rafiki,
Tumetumwa mara ngapi na Mungu?
Hatupeleki ujumbe tuliotumwa na Baba
Kwa ujinga tunadhani twajificha
Hebu leo tuwe kama Yona
Tugeuke na kwenda kufanya kazi
Bwana anatutuma…
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 35, Kurasini Acapella, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments