Panapo Pendo Lyrics sung by Light Group Ministry
Panapo Pendo Lyrics sung by Light Group Ministry
1. Vitu vyote ni sawa, Panapo pendo
Kila sauti tamu, Panapo pendo
Pana amani pale, Na furaha nyumbani
Siku zote salama, Panapo pendo
Chorus
Siku zote salama,
Panapo pendo.
2. Furaha i nyumbani, Panapo pendo
Hapana machukizo, Panapo pendo
Chakula ni kitamu, Mashamba ya sitawi
Maisha ni kamili, Panapo pendo
3. Hata mbinguni juu, Pana furaha
Wakiona upendo, Nyumbani mwetu
Macho yanapendezwa, Na viumbe vya Mungu
Naye Mungu huona, Panapo pendo
4. Ee Yesu niwe wako, Wako kabisa
Ndipo patakuwako, Pendo nyumbani
Nitakaa salama, Sitaifanya dhambi
Nitabarikiwa tu, Panapo pendo.
Light Group Ministry.
Light Group Ministry, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments