Pumzi Ya Uhai Lyrics sung by Hope Voice Group
Pumzi Ya Uhai Lyrics sung by Hope Voice Group
1. Pumzi ya uhai inapotoweka, Mwili ukibaki pekee yake
Pale pale tukiwa tumelala, Neno lasema tumekufa
Pale pale tukiwa tumelala, Neno lasema tumekufa
Refrain
(Kifo) Kifo umetutenga na wazazi,
Umetutenga na watoto wetu
Wapendwa wengi wamelala,
Wanasubiri ufufuo
2. Mwili ukishushwa ndani ya kaburi, Watu wakilia kwa huzuni
Matumaini yao yatoweka, Wengi hawana msaada
Matumaini yao yatoweka, Wengi hawana msaada
3. Tunaye rafiki aloshinda kifo, Aliyefufuka toka kwa wafu
Ndiye Yesu Mwokozi wa dunia, Tukimwamini tutaishi
Ndiye Yesu Mwokozi wa dunia, Tukimwamini tutaishi.
Hope Voice Group.
Hope Voice Group, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments