Wednesday, 22 January 2025

Ungeniambia Nilipokosea Lyrics sung by Acacia Singers

Ungeniambia Nilipokosea Lyrics sung by Acacia Singers


1. Ungeniambia nilipokosea

Nikalijua kosa langu

Uenda ningebadilika

Nikajirekebisha

Umeifanya dhambi yangu

Kunuka mbele za watu

Mdahalo wote juu yangu

Kwa kosa nisilojua


Iiii Iiii Maneno haya yanahuruma

Ungeniambia nilipokosea

Nami nikabadilika


2. Maneno yanayonenwa juu yangu

Yanaumiza roho yangu

Laiti kama ungenijulisha

Nikajua ubaya wangu

Ungeniita kwa upole

Ukanieleza kwa pendo

Ungeiokoa nafsi yangu

Kwa haya yatokeayo 


3. Leo* uamue uje kwa Yesu

Aliye msaada wetu

Hakika Bwana wetu atupenda

Yeye ana huruma nyingi

Hutuonya kwa upole,

"Msitende dhambi wanangu,"

Yeye husamehe, husahau

Wala hakumbuki tena


Outro

Yesu utusaidie tuvishe

*Tufike mbele sote

Tufike mbinguni.


Acacia Singers, Tz.

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...