Thursday, 30 January 2025

Mimi Ni Mungu/Mungu Wa Huruma Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Mimi Ni Mungu/Mungu Wa Huruma Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

1. Mimi ni Mungu wenu asema Bwana
Nirudieni mimi Mungu wa kweli
Mnapotanga mbali nasikitika
Njooni wanangu sasa rudini nyumbani

Refrain
Mungu wa huruma tena mwenye na upendo
Aita wenye dhambi njooni wanangu

2. Yeye ajaye kwangu sitomtupa
Nitampa uzima ule wa milele
Kila asikiaye na aje sasa (asema)
Nyumbani mwake Baba makao ni mengi

3. Wataoshinda dhambi ‘tavikwa taji
Naye Mwokozi Yesu ‘tawakaribisha
‘Ingieni rahani mwa Baba yangu’
Mle mema ya nchi yaloandaliwa

Acacia Singers, Tz.

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...