Sikia Neno La Bwana Yesu Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Sikia Neno La Bwana Yesu Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

1. Sikia neno la Bwana Yesu Alivyosema kwa huzuni,
‘Mikononi mwako Baba yangu. Roho yangu uipokee’
Baada ya hayo Yesu Bwana, Alikataa roho kwa huzuni
Baada ya hayo Yesu Bwana, Alikataa roho kwa huzuni

Refrain
Aliishinda kifo Yesu (wangu) Sasa yu hai Bwana wangu
Yauja tena na Malaika Kila jicho litamuona

2. Na ilipokwisha pambazuka Siku ya kwanza ya juma
Walikwenda tazama kaburi Tazama lilikuwa tupu
Malaika wa Bwana alishuka Akaliondoa lile jiwe
Malaika wa Bwana alishuka Akaliondoa lile jiwe 

3. Ingawa walilinda kaburi askari wote walishindwa
Hofu kuu ilikuja kwao Wakatetemeka kwa uoga
Tetemeko kuu la kutisha Wakaanguka kwa nguvu hizo
Tetemeko kuu la kutisha Wakaanguka kwa nguvu hizo

Acacia Singers, Tz.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA