Nguvu Zangu Pekee Lyrics sung by Acacia Singers
Nguvu Zangu Pekee Lyrics sung by Acacia Singers
1. Nguvu zangu pekee hazitoweza
Kupambana naye Ibilisi
Jeshi lake kubwa huniandama
Kote niendako hunitisha
Refrain
Nakuita mchungaji mwema (Yesu)
Yesu mwana wa Mungu (Kweli)
Nipitapo kati ya nyika
Bwana nisiogope
2. Ewe Mungu wangu nisaidie
Ona nasumbuka na mateso
Mzigo mzito niliobeba
Tautua kwako nipumzike
3. Masumbuko haya mpaka lini?
Bwana wangu Yesu niahidi
Tutapokutana makao mapya
Baba mama wote niwaone
Refrain
Nakuita mchungaji mwema (Yesu)
Yesu mwana wa Mungu (Kweli)
Nipitapo kati ya nyika
Bwana nisiogope
4. Ninapotazama juu mbinguni
Naiona nyota ile tukufu
Tukufu kwa wale wasafirio
Kwa machozi mengi Bwana Yesu
Refrain
Nakuita mchungaji mwema (Yesu)
Yesu mwana wa Mungu (Kweli)
Nipitapo kati ya nyika
Bwana nisiogope.
Acacia Singers, Tz.
Comments
Post a Comment