Wednesday, 22 January 2025

Punda Mwana Punda Lyrics sung by Acacia Singers

Punda Mwana Punda Lyrics sung by Acacia Singers


Chorus

Endendeni katika kile kijiji kile kinachowakabili (Ndipo)

Mtamwona punda kafungwa na mwanapunda

Pamoja naye wafungueni nanyi mnilete

Mkiulizwa semeni Bwana anawahitaji

Mkiulizwa semeni Bwana anawahitaji


1. Wakaenda zao wale wanafunzi

Wakafanya vile alivyowaamuru

Shangwe furaha tele mji wote

Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana

Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana (Sasa)


2. Sababu ya furaha walokuwa nayo

Walitandika nguo zao njia yote

Wakiwa na matawi mikononi

Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwan

Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana (Sasa)


3. Njooni tumwimbie Yesu Bwana wetu

Kwa ushindi mkuu natumtukuze

Njooni tumsifu mkombozi

Huyu ndiye Yesu Mwokozi wa maisha yetu (Haleluya)

Huyu ndiye Yesu Mwokozi wa maisha yetu.


Acacia Singers, Tz.


Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...