Makaoni Mwake Lyrics sung by Acacia Singers

Makaoni Mwake Lyrics sung by Acacia Singers

1. Makaoni mwake Bwana nitaketi
Nile naye, nizungumze naye
Furahani mwake Bwana nitaketi
Nimwimbie wimbo mutamu
Nikiwa na amani na furaha moyoni mwangu
Nikiwa na amani na furaha moyoni mwangu

Refrain
Furaha yangu nifike juu
Yesu Mwokozi anipokee
Nitaimba na Malaika
Nyimbo nzuri nikimsifu Bwana

2. Mji wake Mungu niutamanio
Kuna raha isiyo kifani, aah
Wote walochoka watapumzishwa
Yesu Kristo atawafariji (kweli)
Kwenye mji wa Mungu ‘taishi naye Bwana wangu
Kwenye mji wa Mungu ‘taishi naye Bwana wangu

3. Tutakusanyika toka kila pembe
Kulitukuza jina la Yesu
Malango ya lulu yatafunguliwa
Naye Yesu Mkombozi wetu
Sikia nikueleze kuna raha kule kwa Baba
Sikia nikueleze kuna raha kule kwa Baba

Acacia Singers, Tz.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA