Huyu Yesu Mnazorayo Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Huyu Yesu Mnazorayo Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Verse 1
Huyu Yesu, ataitwa mnazorayo
Huyu Yesu, ataitwa mnazorayo
Twakueleza habari zake Yesu
Aliyeishi kama maskini
Akalelewa Yesu mjini Nazareti
Wakaazi wa mji huo
Wakamwita mnazorayo

Ata akakuwa akihubiri kote
Neno la uzima katika miji yote
Ata akakuwa akihubiri kote
Neno la uzima katika miji yote

Aliitwa mnazorayo
Aliitwa mnazorayo

Verse 2
Alikamatwa Yesu mnazorayo
Akapelekwa mbele ya makuhani
Akaeleza Yesu, “Nalikuwa nanyi,
Siku zote hekaluni nikiwafundisha nyote
Lipi nililotenda kwenu watu wangu
lililobaya kwenu nanyi mwanikamata?
Lipi nililotenda kwenu watu wangu
lililobaya kwenu nanyi mwanikamata?”

Break
Aaa-uuh, Aaah-Aaah
Aaa-aah, Aaah-Uuuh-Aliteswa!

Verse 3
Aliteswa Yesu mnazorayo
Aliteswa Yesu mnazorayo

Akaangikwa pale juu Goligotha
Yesu kalia Eloi, Eloi, Lama Sabakthani?"
Yaani "Mungu wangu,
Mbona sasa waniacha,"
Alilia Yesu masikini

Taji ya miba kawekewa kichwani
Wale Wayahudi hawakumfahamu
Taji ya miba kawekewa kichwani
Wale Wayahudi hawakumfahamu

Verse 4 Outro
Isingekuwa kifo chake Yesu
Nani angetoa uhai wake?
Isingekuwa kifo chake Yesu
Nani angetoa uhai wake?

Verse 5 Outro
Nani mwenye huruma kama Mungu wetu
Kumtoa mwana kubeba laana yangu *4

Acacia Singers, Tz.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Damu Yake Lyrics sung by The Golden Gate Choir

Nyosha Mkono Wako Lyrics sung by Nyandema SDA Choir