Thursday, 7 May 2026

Mwovu Shetani Ametawala Dunia (Rushwa) Lyrics sung by Betheli AY Choir

Mwovu Shetani Ametawala Dunia (Rushwa) Lyrics sung by Betheli AY Choir


1. Mwovu Shetani ametawala dunia,

Ameshika wengi katika nyavu zake;

Za kiburi na umimi.

Watu wengine wapenda wapewe ulimwengu wote;

Kwa gharama yote ile

Wanatoa rushwa ili kuwanyanyasa wengine.


Refrain

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Inaua haki yote

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Haipendezi Yehova

Rushwa inazidisha kiburi umimi

Rushwa inaongoza kwa kila dhambi

Atoae rushwa na anayepokea

Wote watahukumiwa na Mungu.


2. Rushwa yatolewa kwa njia mbalimbali

Kwa kutoa pesa kunyang'anya haki wanyonge (Na Kushawishi)

Kushawishi (Ooh) wengine ili pia nao washuhudie uhongo

Kama Ahabu (Kama Ahabu) kwa Nabothi, (Kwa Nabothi)

Lakini Mungu yeye hatolewi rushwa.


Refrain

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Inaua haki yote

-(Ooh Rushwa, Rushwa, Rushwa kazini)

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Haipendezi Yehova

--(Rushwa Inaua, Tuachane na Rushwa, Tuepuke Rushwa)

Rushwa inazidisha kiburi umimi

Rushwa inaongoza kwa kila dhambi

Atoae rushwa na anayepokea,

Wote watahukumiwa na Mungu.


3. Mungu wetu ni mkamilifu na haki,

Hatakubali uovu kutawala milele

Walionyimwa haki yao,

Kwa ajili ya rushwa Mungu yeye anaona 

Atatoa hukumu ya haki,

Kwa matendo yetu yale yasiompendeza.


Refrain

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Inaua haki yote

-(Ooh Rushwa, Rushwa, Rushwa yaua)

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Haipendezi Yehova

--(Rushwa kazini, Rushwa hospitalini, Hata kanisani)

Rushwa inazidisha kiburi umimi

Rushwa inaongoza kwa kila dhambi

Atoae rushwa na anayepokea

Wote watahukumiwa na Mungu.


Rushwa inazidisha kiburi umimi

Rushwa inaongoza kwa kila dhambi

Atoae rushwa na anayepokea

Wote watahukumiwa na Mungu.


Rushwa! Rushwa! Rushwa! Inaua haki yote

-(Rushwa, Rushwa, Rushwa, Haipendezi Yehova, Rushwa)

Rushwa! Rushwa! Rushwa! Haipendezi Yehova.


Betheli AY Choir.


Betheli AY Choir, SDA Kiswahili Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...