Itakuwa Kutano Kuu
Lyrics Sung by Acacia Singers, Tz
1. Itakuwa kutano kuu, ambalo
halitahesabika
Ni wale wale wamealikwa, Yesu
atakuwa nao
Nabii wa Mungu alionyeshwa,
kutano kuu wa ajabu
Ambalo mtu hawezi hesabu, ili
kujua idadi yake
Umati mkubwa tena sana, Watu wa
mataifa mbali mbali
Yesu Bwana, Yesu Bwana, atakuwa kati
yao
Yesu Bwana, Yesu Bwana, atakuwa kati
yao.
Refrain
Waliokombolewa watakuwa wengi
sana,
Sawa na mchanga wa bahari
Ambao mtu hawezi hesabu,
Kwa wataokombolewa, je utakuwepo?
2. Nao watakatifu wataanguka (Wote),
Mbele ya kiti cha enzi
Kumsujudu Mungu Mwenyezi, Aliyeumba
mbingu na nchi
Baraka utukufu, hekima,-? Mungu
wetu mtawala
Mtukufu! Mtukufu! Astahili Mungu
wetu
Mtukufu! Mtukufu! Astahili Mungu
wetu.
3. Taji zitang'aa kwao washindi (Wote),
Waimba nyimbo za sifa
Mikononi mwao wana mitende, Washangilia
kwa shangwe kuu (Kweli)
Ebu jiulize kwa makini, Utakuwa
wapi siku hiyo?
Ndugu yangu tafakari mbona,…?
cuts off –
This song cand be found in YouTube.
Note & For Revision: Baraka
utukufu, hekima,-? Mungu wetu mtawala
Acacia Singers Tz Mwenge, SDA Swahili Songs, Bedi Score, Bedi Lyrics