Ninakaza Mwendo (Jubili) (Jubilee) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Ninakaza mwendo nifike, kwenye Jubili mbinguni
Japo vikwazo ni vingi, vyote vyaniimarisha
Nasafiri kwenda kwa Baba, sitaki kurudi nyuma
Hapa nilipofikia, sasa, yatosha niwe huru
Refrain
Jubili, Jubili, Jubili ya wateule,
Ni mimi na wewe tunaalikwa
Wanaimba nyimbo za ushindi,
Wakiongozwa na Yesu,
Wamesahau machungu yote,
Jubili ya wateule
2. Nitakapofika mbinguni, uso kwa uso na Yesu
Machungu yametoweka, niko kwenye utukufu
Sasa siwezi kueleza, jinsi itakavyokuwa
Hapa nilipofika, sasa, yatosha nipumzike.
Note: Wanaimba nyimbo za ushindi; Brings the future to the present moment. The Saints are singing; The Saints are singing.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 30, Bedi Score, Bedi Lyrics