Leteni Zaka Kamili Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Leteni zaka kamili na sadaka, mpate kubarikiwa na Mungu
Tena msilete iliyo dhaifu, Mungu hapendezwi kabisa
Wala msilete kwa manung'uniko mzipate baraka zake
Nani kati yenu amefilisika, kwa kumtolea Mungu?
Refrain
Fungueni, fungueni, fungueni hazina zenu
Fungueni, fungueni, mahali palipo salama
Fungueni, fungueni, fungueni hazina zenu
Fungueni, fungueni, mahali palipo salama.
2. Baraka za Bwana zimejaa tele, kwa atoae kwa uaminifu
(Tena) Mnaweka hazina kwenye mifuko, mifuko iliyotoboka
Mjaribu Bwana nawe utaona, mibaraka ameahidi
Wekeni hazina zenu juu mbinguni, pahali pa salama.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 30, Bedi Score, Bedi Lyrics