Monday, 11 May 2026

Yesu Alipokuwa Lyrics Sung by Your Voice Melody

Yesu Alipokuwa Lyrics Sung by Your Voice Melody


Pre-Chorus

Yesu alipokuwa njiani kwenda Yerusalemu,

Alipitia Samaria na Galilaya

Alipoingia ndani ya kijiji kimoja,

Alikutana na watu kumi wenye ukoma

Walisimama mbali naye (--Na-ye-- Yesu),

Wakapaza sauti wakisema uturehemu


Alipowaona, aliwaambia,

‘Endeni mkajionyeshe kwa makuhani

Na walipokuwa wakienda walitakasika.

Walipaza sauti wakisema,

‘Eeh Yesu Bwana mkubwa uturehemu.’


Chorus II

Mmoja wao alipoona kwamba amepona,

Alirudi kwa Yesu akiwa na furaha tele

Kamshukuru Bwana,

Kampa utukufu,

Imani yake ilimuokoa.


Mmoja wao alipoona kwamba amepona,

Alirudi kwa Yesu akiwa na furaha tele

Kamshukuru Bwana,

Kampa utukufu,

Imani yake ilimuokoa.


Verse

Watu wengi wanasahau

Wanasahau,

Yale Mungu amewatendea

Binadamu,

Binadamu hana asante,

Kwa yale Mungu ametenda


Ni mara ngapi we, Mungu amekuponya?

(----------------------------------------Amekuponya we)

Ni mara ngapi amekutoa shimoni?

(-------------------------Amekutoa shimoni?)


Tabia ya mwanadamu akiwa na shida

(--------ya mwanadamu---akiwa na shida)

Anamkumbuka Mungu akipata anamsahau,

(------------------------------akipata anamsahau)


Tabia ya wanadamu tukiwa na shida,

(--------ya wanadamu---------na shida)

Tunamkumbuka Mungu tukipata tunamsahau

(-------------------------------tukipata tunamsahau)


Shukuru Mungu kwa kila jambo,

Jifunze kusema asante ndugu yangu


Pre-Chorus

Yesu alipokuwa njiani kwenda Yerusalemu,

Alipitia Samaria na Galilaya

Alipoingia ndani ya kijiji kimoja,

Alikutana na watu kumi wenye ukoma

Walisimama mbali naye (--Na-ye-- Yesu),

Wakapaza sauti wakisema uturehemu


Alipowaona, aliwaambia,

‘Endeni mkajionyeshe kwa makuhani’

Na walipokuwa wakienda walitakasika.

Walipaza sauti wakisema,

‘Eeh Yesu Bwana mkubwa uturehemu.’


Chorus II

Mmoja wao alipoona kwamba amepona,

Alirudi kwa Yesu akiwa na furaha tele

Kamshukuru Bwana,

Kampa utukufu,

Imani yake ilimuokoa.


Mmoja wao alipoona kwamba amepona,

Alirudi kwa Yesu akiwa na furaha tele

Kamshukuru Bwana,

Kampa utukufu,

Imani yake ilimuokoa.


Your Voice Melody.


Your Voice Melody, SDA Swahili Songs, SDA Swahili Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...