Zamani Watoto (Soma Soma) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Pre-Verse
Zamani watoto walikwenda kwa Yesu,
Yesu kawabariki
Wanafunzi walitaka kuwazuia,
Yesu kawakemea.
1. Tafuta elimu usiiachi, Itakuacha mbali ndugu
Elimu ni chanzo cha kumjua Mungu,
Wapee watoto elimu, wamjue Mungu
‘Waache waje kwangu,’ asema Bwana.
Refrain
Tafuta elimu ndugu,
---Soma, soma, soma
Upate kumjua Mungu,
---Soma, soma, soma
Utapeleka injili,
Nenda watu waangamia kwa kukosa maarifa.
2. Elimu ufunguo wa maisha, Tuwape watoto elimu,
Leeni watoto kwa njia ipasayo,
Nao hawatasahau, wamjue Mungu
‘Waache waje kwangu,’ asema Bwana.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Vol 27, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics