Tuesday, 2 June 2026

Umekwisha Sikia Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Umekwisha Sikia Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Umekwisha sikia kisa cha Musa,

Habari za Daudi na Kombeo,

Kisa cha Yusufu na ndoto zake,

Na Yona ndani ya tumbo la samaki,

Pamoja na wengi wa siku za kale

Ninatamani kuonana nao,

Kwa uwezo wa Bwana nitawaona, siku ile ajapo.


Refrain

Kutakuwa na mkutano juu angani, Bwana anaporudi

Tutakutana kule pamoja nyumbani juu angani

Tutaimba wimbo wa Musa na Mwanakondoo,

Siku ile ya utukufu

Naye Yesu atatuongoza, tukikutana sote.


2. Mambo mengi yatakosekana pale,

Hakutakuwepo maombolezo,

Hakuna tena Wokovu kwa wadhambi,

Wito wa Yesu waliukataa

Hakuna huzuni hakuna upweke

Hakuna mizigo tena mioyoni

Hayo yote Bwana Yesu atafuta, siku ile ajapo.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir Vol 27, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare 1. Ndoa ilibarikiwa na Mungu , Ilianza pale Edeni Kwani Mungu aliona, si vyema Adamu , Awe pek...