Tuesday, 2 June 2026

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare


1. Ndoa ilibarikiwa na Mungu,

Ilianza pale Edeni

Kwani Mungu aliona, si vyema Adamu,

Awe pekee yake msaidizi.


Refrain

Waliounganishwa naye Muumba

Mwanadamu yeyote asiwatenganishe

Kwani siku ya leo ni siku ya raha,

Mnapozifunga pingu za maisha.


2. Ndoa inatuonyesha pendo la Mungu,

Wanandoa mpendane

Katika mambo yote, mmyapitiayo,

Huku mkimtanguliza Muumba.


Diana Gesare.


Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ndugu Unaposema (Ubatizo) Lyrics sung by Diana Gesare

Ndugu Unaposema (Ubatizo) Lyrics sung by Diana Gesare


1. Ndugu unaposema kwamba umebatizwa,

Imekupasa kuyachunguza sana maneno yako

Kwani ubatizo una maana ya kuzamisha,

Alivyozamishwa Mwokozi wetu Yesu mtoni Yorodani

Alivyozamishwa Mwokozi wetu Yesu mtoni Yorodani.


Refrain I

Uzamishwa ndani ya maji, maji yalo mengi

Ni ishara ionyesha kufa na kufufuka.


Refrain II

Ndiyo ubatizo ulio wa kweli,

Hebu na tufuate nyayo za Bwana Yesu.


2. Tuna Baba mmoja, Biblia ni moja, Imani moja

Na njia nayo ni moja, ambayo ni Yesu

Mbona tusizifuate nyayo zake Mwokozi?

Kwa kubatizwa alivyobatizwa Bwana Yesu mtoni Yorodani

Kwa kubatizwa alivyobatizwa Bwana Yesu mtoni Yorodani.


3. Ubatizwapo ndugu, kumbuka ni ishara,

Ya kuyazikwa mambo yale ya zamani yalo ya giza

Ebu mwamini leo ufanye uamuzi

Ili uzaliwe mara ya pili uwe kiumbe kipya

Ili uzaliwe mara ya pili uwe kiumbe kipya.


Diana Gesare.


Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare 1. Ndoa ilibarikiwa na Mungu , Ilianza pale Edeni Kwani Mungu aliona, si vyema Adamu , Awe pek...