Friday, 6 September 2024

Nikikumbuka Huruma Yako (Yanipasa Nikakutumikiye) Lyrics sung by The Golden Gate Choir

Nikikumbuka Huruma Yako (Yanipasa Nikakutumikiye) Lyrics sung by The Golden Gate Choir


1. Nikikumbuka huruma yako ewe Bwana Yesu

Nikikumbuka mahali ambapo nilikutwa mimi

Nikikumbuka matendo mema uliyoonyesha

Yanipasa nikakutumikiye

Yanipasa nikakutumikiye


Chorus

Nitakuimbia wimbo wangu mpya

Nikutumikie kwa kuokolewa (Eh Bwana)

Nikumbuka maovu mengi niliyoyatenda

Yanipasa nikakutumikiye

Yanipasa nikakutumikiye


2. Nikikumbuka matendo mema unionyeshayo

Kwa kutoka mbinguni kwako ukaniokoe

Maumivu msalabani hata kifo chako

Yanipasa nikakutumikiye

Yanipasa nikakutumikiye


3. Nikikumbuka sauti yako iliyosikika

Nikukumbuka heshima yako kule juu mbinguni

Uliumba ulimwengu, watu hata ndege

Yanipasa nikakutumikiye

Yanipasa nikakutumikiye.


The Golden Gate Choir.


The Golden Gate Choir, Mukalu Kaggwa Isaac, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...