Hatujui Saa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir
Hatujui Saa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir
1. Hatujui saa ya kuja kwa Bwana Yesu,
Lakini dalili zasema hivi karibu
Atakaporudi na ufalme wake
Lakini kwa kweli Hatujui saa yake
Refrain
Atakuja, kwa vile tukeshe na kuomba;
Atakuja Mwokozi, Haleluya!
Atakuja kwa fahari ya Baba yake,
Hatujui saa ya kuja kwake Kristo.
2. Pana nuru kwa wale wapendao haki,
Pana kweli katika chuo chake Mungu;
Unabii hufundisha kuja kwake Bwana,
Lakini hatujui saa yake Kristo.
3. Tutakesha na tutaimba daima ndugu,
Tutafanya kazi mpaka akija Bwana,
Tutaimba na tutasoma ishara zake,
Hatujui saa ya kuja kwa Mwokozi.
Nyandema SDA Choir.
Re 22:12 And, behold, I come quickly; and my reward is with me, to give every man according as his work shall be.
Re 16:15 Behold, I come as a thief. Blessed is he that watcheth, and keepeth his garments, lest he walk naked, and they see his shame.
Mt 25:13 Watch therefore, for ye know neither the day nor the hour wherein the Son of man cometh.
Comments
Post a Comment