Mlango Ni Wazi Kwa Wenye Dhambi Lyrics sung The Golden Gate Choir
Mlango Ni Wazi Kwa Wenye Dhambi Lyrics sung The Golden Gate Choir
1. Mlango ni wazi kwa wenye dhambi
Yesu ndiye anawaita
Anahurumia waliokosa
Wafikishe kwake ulimwenguni
Furaha ni nyingi kwake mwokozi
Tutakapofika mbinguni
Tutamwimbia nyimbo za shangwe
Tumsifu mwokozi - Yesu
Chorus
Tutapokea taji kwa Yesu - kwake Yesu
Mara tutakapofika mbinguni - mbinguni kwake
Tutamwimbia nyimbo za shangwe
Tumsifu mwokozi - Yesu
2. Ni maji ya bure chota uyanywe
Haya maji ni ya uzima
Njoo uyapokee uponye kiu
Uwe hai kwake milele
Furaha ni nyingi kwake mwokozi
Tutakapofika mbinguni
Tutamwimbia nyimbo za shangwe
Tumsifu mwokozi, Yesu
3. Utapumuzika kwake milele
Pamoja na Yesu mbinguni - kwetu
Utakaribishwa u'pewe zawadi
Ndio uzima wa milele
Furaha ni nyingi kwake mwokozi
Tutakapofika mbinguni
Tutamwimbia nyimbo za shangwe
Tumsifu mwokozi, Yesu.
The Golden Gate Choir.
The Golden Gate Choir, Mukalu Kaggwa Isaac, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments