Nilikaa Katika Upweke Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA
Nilikaa Katika Upweke Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA
1. Nilikaa katika upweke katika giza la huzuni
Nilijaribu kutafakari Juu ya maisha haya upweke
Kumbe kando alikuwepo Mungu asikizaye maombi
Refrain
kwa hii leo amenijibu Ombi hilo nikatisha tamaa
Kwa hii sasa nasadiki Mungu hakawii 'timiza ahadi
2. Pengine umeshasumbuka Na moyo umeshavunjika
Kila uendako ni giza tu Natumai' limeshatoweka
Fikiria Yesu alivyo omba Yakatoka matone ya damu
3. Moyo wangu *umetulizwa Sina hofu juu ya faraja
kwa hii wewe ndiwe kimbilio Na wokovu wa maisha yangu
Shida taabu zinisongapo Nitaku tazama Mwokozi
Cherubim Singers, Nairobi South SDA.
*umetulizwa = Not very clear. ?umejulizwa
Comments
Post a Comment