Yesu Mwokozi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA
Yesu Mwokozi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA
1. Yesu mwokozi Yesu mwokozi
Nakulilia mimi mwenye dhambi
Na kwa sababu ya unyonge wangu Bwana
Naja kwako Bwana unirehemu
[Asante] Asante kwa kunikomboa mimi
kwa damu yako na dhamani
[Bwana] Nilinde ni wako Bwana wangu
Niwe chombo kamilifu kwako
2. Japo dhoruba zijatusonga
Twaegemea kwako ewe Bwana
Wewe ni ngome na kimbilio letu
Mwamba uliye imara daima
3. Ahadi zako ni za milele
Twatazamia kuja kwako Bwana
Ili tuende nawe kule mbinguni
Tukaishi nawe siku zote.
Cherubim Singers, Nairobi South SDA.
Comments
Post a Comment