Tulipofika (Kila Goti Litapigwa) - Wastahili Heshima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Tulipofika kwenye miamba ya kutisha,
Yesu akawa ni mwamba wa kale
Tulipovuka bahari (bahari), Yesu maji ya uzima
Kwenye wanyama wakali (wakali), Kaitwa simba wa Yuda
Alipofika kwa wenye wadhambi,
Wakamwita Imanueli Mungu pamoja nasi

Refrain
Kila goti litapigwa litapigwa
Hakika mchana kweupe
Kila ndimi litakiri likisema,
Wazi wewe mwana wa Mungu
Wastahili heshima leo,
Hata milele milele

2. Tutakapofika mbinguni tutamuona,
Itakuwa ni furaha ajabu
Kufumba na kufumbua (fumbua), Makovu yataponyeshwa
Majeruhi watapona ('tapona), Hakuna maombolezo
Tutakapofika kwenye meza ya fahari,
Imanueli atakuwa wa kwanza.

Kurasini SDA Choir.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA