Monday, 22 September 2025

Apandaye Haba Lyrics sung by Grace and Glory Singers

Apandaye Haba Lyrics sung by Grace and Glory Singers

Chorus
Apandaye haba atavuna haba
Na apandaye kwa ukarimu ni ukarimu
Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake
Si kwa huzuni wala si kwa lazima
Maana Mungu humpenda yeye
Atoaye kwa moyo wa ukunjufu
Tena ni mwenye heri

Verse 1
Leteni zaka kamili ghalani
Ili kimo chakula katika nyumba yangu
'Mkanijaribu kwa njia hiyo
Asema Bwana wa majeshi'
Mjue kama sitawafungulia 
Madirisha yote ya mbinguni
Na kuwamwagieni baraka za mbingu
Hata isiwepo nafasi ya kutosha

Chorus
Apandaye haba atavuna haba
Na apandaye kwa ukarimu ni ukarimu
Kila mtu na atende
Kama alivyokusudia moyoni mwake
Si kwa huzuni wala si kwa lazima
Maana Mungu humpenda yeye
Atoaye kwa moyo wa ukunjufu
Tena ni mwenye heri

Verse 2
Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe
Bali kamtoa kwa ajili yetu si’ sote
Atakosaje kutukirimia
Na mambo yote, pamoja naye.

Chorus
Apandaye haba atavuna haba
Na apandaye kwa ukarimu ni ukarimu
Kila mtu na atende
Kama alivyokusudia moyoni mwake
Si kwa huzuni wala si kwa lazima
Maana Mungu humpenda yeye
Atoaye kwa moyo wa ukunjufu
Tena ni mwenye heri.

Grace and Glory Singers.

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...