Bwana Twataka Njia (Ukuta Wa Jeriko) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Bwana twataka njia kwenda ng’ambo
Mbele yetu kuna vikwazo vingi
Jeshi la Bwana limeshapanga vita
Lataka kuvuka Makedonia
Kama Paulo na Sila waliomba
Lango la gereza likafunguka
Refrain
Ukuta wa Jeriko (Jeriko)
Ulibomoka kwa nguvu za Mungu
Tutakaa kimya Bwana atapigana
Ukuta utasambaratika
Nahodha wetu ni Yesu yuko mbele
Njia nyeupe tupite
Jina la Yesu ni kama ngao kwenye vita
Twataka kuvuka watu wanaangamia
2. Mbiu imelia jeshi vitani
Uria amerudishwa nyumbani
Uria kwa kinywa chake akasema,
‘Talalaje jeshi liko vitani (Bwana)
Fungua njia Bwana tusonge mbele
Yowe limelia kwapambazuka.
Kurasini SDA Choir.
Comments