Giza Nene Limetanda Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Giza nene limetanda usoni
Napapasa sioni pa kushika
Msaada wangu ‘tatoka wapi?
Natafuta uso wa Bwana wangu
Anishike mkono nifike kwake
Refrain
Sauti ikasema mimi ni Mungu wako
Ni Alfa na Omega Mwanzo mwisho
Niite wakati wa shida,
Mimi nitajibu, (Kwa kweli nitajibu)
‘Katika mambo magumu niite (Mimi)
Tangu mwanzo nilikuwepo (Mimi nipo)
Leo nipo (Leo nipo) kesho nipo (Kesho nipo) niite kwako
Mambo magumu kwako Nitajibu Niite nitaitika,
Mambo magumu kwako Nitajibu Niite nitaitika’
2. Majaribu yaliyo mbele yangu
Kila siku ninapanda kushuka
Kila siku ninayaona mapya
Msaada wangu ‘tatoka wapi?
Natafuta uso wa Bwana wangu.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Ukuta Wa Jeriko Album, Bedi Score, Bedi Lyrics