Kama Wanaisraeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers
Kama Wanaisraeli Lyrics sung by Grace and Grory Singers
1. Kama Wanaisraeli Katika safari yao
Safari ya siku chache jangwani Ikawa ya miaka mingi
Wengi walikata tamaa Wengi walifia njiani
Ni wachache walifika Nchi ya ahadi
Ni wachache walifika Nchi ya ahadi
Refrain
Tutembee kwa ujasiri Kwenye safari ya Kaanani
Yesu nahodha wetu ‘tatuvusha salama
Bila mwongozo wake Hatuwezi vuka mto Yordani
Tujipe moyo tutafika
2. Nasi tunapiga hatua Moja mbele mbili nyuma
Katika safari yetu ya mbingu Tupatapo majaribu
Tukazeni mioyo yetu sasa Tufikie ng'ambo ya pili
Kwani Pwani sio mbali Mwisho tutafika
Kwani Pwani sio mbali Mwisho tutafika.
Grace and Glory Singers.
Comments