Kati Ya Vyote (Aliniumba Kwa Mfano Wake) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Kati Ya Vyote (Aliniumba Kwa Mfano Wake) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Kati ya vyote vilivyoumbwa,
Niliumbwa kwa mfano wa Mungu
Ni kwa sababu alinifinyanga
Kwa mfano wake, Eeeh-Eeeh-Eeeh
Nilitoka mikononi mwake,
Inapendeza kurudi kwake
Aliniumba kwa mfano wake,
Kwa mapenzi ya Mungu
Refrain
Aliniumba kwa mfano wake,
Inapendeza nilitoka kwake
Ingawa dhambi ilitia waa,
Aliniosha nikawa safi
Ingawa dhambi ilitia waa,
Aliniosha nikawa safi, Safi-ii safi-ii
Aliniosha nikawa safi, Safi-ii safi-ii,
Aliniosha nikawa safi
2. Kanipulizia pumzi yake,
Nipate kuwa kiumbe hai
Ni kwa sababu alinifinyanga
Kwa mkono wake, Ooh-Ooh-Ooh
Ndio sababu ninapendeza,
Kuliko vyote vilivyoumbwa
Aliniumba kwa mfano wake,
Kwa mapenzi ya Mungu.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Ukuta Wa Jeriko Album, Bedi Score, Bedi Lyrics
Comments