Katikati Ya Mafarao (Amini) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


Yuko Mungu atakae simama kwa ajili yako
Immanueli Mungu yupo nasi
Ebeneza Mungu wa maajabu
Atakuinulia uso wake
Akufadhili akulinde
Malaika wakuzunguka kote
Uko mikononi mwake

Refrain
Amini, (Amini) na tena uamini
Anashughulikia maisha yako
Amini, (Amini) na tena uamini
Rehema zake kwako ni za ajabu
Uamini na tena uamini
Maisha yako mikononi mwake
Uamini na tena uamini
Roho anaugua kwa ajili yako

2. Katikati ya masumbuko yako
Yuko anayeweza kukuonyesha
Upendo uliokwisha toweka
Faraja kwa wanaoteseka
Yuko Mungu anayejali leo
Atakuwa mfariji kwa waliokataa tamaa
Waliosongwa na dunia hii
Walimwengu watakapokushusha
Atakufunika mbawani mwake
Ujisalimishe kwake.

Kurasini SDA Choir.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA