Kila Mtu Awapotezea Lyrics sung by Grace and Glory Singers
Kila Mtu Awapotezea Lyrics sung by Grace and Glory Singers
1. Kila mtu awapotezea wenye haki
Katika njia mbaya ataanguka
Katika rima lake yeye mwenyewe
Bali wakamilifu wataridhi mema
Yeye aligeuzaye sikio lake
Asisikie sheria ya Mungu
Hata sala yake ni chukizo,
Chukizo kwa Mungu
Chorus
Basi simameni katika njia kuu, Mkaone,
Mkaulize mapito ya zamani
Iwapo njia iliyo njema,
Mkaenende katika njia, Njia hiyo nzuri
Mkatubu dhambi zenu, Mkawe safi
Naye ninyi basi-ii, Mtajipatia raha katika nafsi zenu
2. Afichaye dhambi zake Hatafanikiwa
Bali yeye aziungamae na kuziacha atapata rehema
Aendaye kwa unyofu ataokolewa
Ila mkaidi wa njia zake Ataanguka mara.
Grace and Glory Singers.
Comments