Malaika Mbinguni (Sauti Za Shangwe) - Unastahili Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Malaika Mbinguni (Sauti Za Shangwe) - Unastahili Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
I
Verse
Malaika mbinguni zikiimba kwa furaha
Watakuwa watakatifu
Watakuwa watakatifu wakiimba
Watapendeza watavutia
Kwa mavazi meupe watapendeza
Verse
Utapenda kuwa mmoja
Utapenda kuwa mmoja wa watakaoimba
Wataimba wimbo mpya
Wakizunguka kiti cha enzi
Wataimba wimbo mpya
Verse
Unastahili Unastahili kuupokea utukufu
Unastahili Unastahili uliimwaga damu
Kukomboa wengi,
Unastahiliiii…
II
Verse
Ulifundisha mitume neno lako
Ukawatuma kufundisha wengine
Walihubiri na kulitangaza neno
Ukawa mwanzo wa injili yako leo
Verse
Injili yako ikatangazwa
Ikafundisha neno lako kwa upendo
Walihubiri habari za mbinguni
Wakawavuta wengi wakujue wewe
Injili yako ikatangazwa kwa upendo
III
Verse
Kazi ni yako Bwana
Uliyotuagiza, ‘Nendeni ulimwenguni kuhubiri
Mkawafanye wote kuwa wanafunzi
Mkiwabatiza kwa jina la Baba,
Mwana na roho mtakatifu,
Nitakuwa nanyi siku zote
Hata ukamilifu na mwisho wa dahari
Mimi niko pamoja nanyi siku zote’
Verse
Unastahili unastahili kuupokea utukufu
Unastahili unastahili uliimwaga damu yako
Kukomboa wengi,
Unastahiliiii…
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Ukuta Wa Jeriko Album, Kurasini Acapella, For Revision, Bedi Score, Bedi Lyrics
For Revision; Review the flow/and presence or absence of certain words in transition.
Comments