Msiwape Mbwa Lyrics sung by Grace and Glory Singers
Msiwape Mbwa Lyrics sung by Grace and Glory Singers
1. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu
Wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe
Wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao
Wakageuka na kuwararua
Omba tafuta bisha, Kwa maana
Kila aombaye hupokea, Naye atafutaye huona
Abishaaye atafunguliwa, Mambo yatakuwa shwari
Kila aombaye hupokea, Naye atafutaye huona
Abishaaye atafunguliwa, Mambo yatakuwa shwari
Chorus
Basi ninyi salini hivi,
Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme,
Ufalme wako uje
Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani, Kama mbinguni
Utupe leo riziki yetu,
Utusamehe deni zetu,
Kama sisi tuwasameavyo wadeni wetu
Usitutie majaribuni
2. Basi msalipo msiwe kama wanafiki
Kwa maana wao wapenda kusali
Hali wamesimama masinagogi na katika pembe za njia
Ili waonekane na watu
Bali wewe usalipo ingia katika chumba chako
Usali mbele ya Baba yako aliye sirini,
Na Baba yako aonaye sirini, Atakujali
Bali wewe usalipo ingia katika chumba chako
Usali mbele ya Baba yako aliye sirini,
Na Baba yako aonaye sirini, Atakujali.
Grace and Glory Singers.
Comments