Piga Kelele Binti Israeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers
Piga Kelele Binti Israeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers
1. Piga e binti Zayuni piga kelele Israeli
Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,
E binti Yerusalemi,
Bwana ameziondoa hukumu zako
Mfalme wa Israeli
Yu katikati yako hutaogopa uovu tena
Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote,
E binti Yerusalemi,
Bwana ameziondoa hukumu zako
Mfalme wa Israeli
Yu katikati yako hutaogopa uovu tena
Refrain
Achumaye juani hula kivulini
Mvumilivu hula mbivu
Tuyavumilie ya dunia japo ni machungu
Si kitambo Yesu arudi
Na tushike ufalme wake
2. “Nitawakusanya wanaousikitia mkutano wa ibada
Nitamponya yeye achechemeaye
Nitamkusanya yeye aliyefukuzwa
Nami nitawafanya sifa na raha
Miongoni mwa watu wote duniani
Nitawapa raha,” asema Bwana.
Grace and Glory Singers.
Comments