Tafakari Kisa/Kisa Cha Wanaisiraeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers
Tafakari Kisa/Kisa Cha Wanaisiraeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers
1. Tafakari kisa cha wanaisiraeli
Walipozunguka zunguka kuta za Yeriko
Kuta zikaporomoka
Si kwa zana za vita wala bomu
Ila kwa vinubi vilivyopulizwa
Kwa uwezo wa Mungu (Kwa kweli) kuta zikaporomoka
Refrain
Waimbaji tupaze sauti zetu
Tuvunje ila zote za mwovu
Wahubiri tangazeni neno
Watu watambue Mungu ni muweza
2. Tumepewa mamlaka naye Mungu wetu
Juu ya vitu – vitu vyote ulimwenguni
Tusiwe na hofu tena
kwa imani tutayashinda yote
Roho wake Mungu yu nasi
Katika majaribu yote, Tuamini kwake Mungu.
Grace and Glory Singers.
Comments