Watu Wengi Walikuja (Waliofika Kwake) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Watu wengi walikuja kwa Yesu
Hawakubakia kama mwanzo
Walibadilika wakazaliwa upya
Jaribu leo utabadilika
Refrain
Waliofika kwake (fika kwake) Wakiwa ni vipofu (vipofu)
Walifanyika wana (wana wana) Wana wa kifalme
Waliofika kwake (fika kwake) Wakiwa ni viwete (viwete)
Wakatupa magongo (yao, yao) Wakaenda zao
2. Namtafuta atakayenitoa hapa, yuko wapi?
Nimezungukwa na adui kotekote, n’ende wapi?
Namtafuta Yesu Ni Yesu pekee wa kunitoa hapa
Namtafuta atakayenitoa hapa, Yesu pekee.
3. Nimezunguka kotekote Ili nimuone Yesu
Kama Zakayo alitamani kumuona Yesu
Akagundua ufupi wake Akapanda juu ya mkuyu
Yesu akamuona kamwambia,
‘Shuka, Wokovu umefika kwako.’
Kurasini SDA Choir.
Comments