Safari Ndefu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Safari ndefu ya injili
Njia ni nyembamba tena imesonga (Kwa kweli)
Hapo ndipo ninatambua sauti ya Bwana
Songa mbele paza sauti (Ondoka)
Watu wangu waangamia,
Nani leo atasimama kwenye zamu yake?
Refrain
Nitajipanga kijasiri (Imara)
Kwenye safari ya injili
Ninajipanga sawa sawa Yesu yuko mbele
Bwana amenipa mamlaka (Mamlaka)
Siwezi kurudi nyuma
Safari iko palepale Vita ni vya Bwana
2. Nitasimama kwenye neno
(Hum-Hum; X2)
Nitasonga mbele njia ya injili (Kwa kweli)
(Hum-Hum; X2)
Dunia ipate kujua Yesu anarudi
Nitasimama kijasiri (Simama)
Watu wangu waangamia,
Nani leo atasimama kwenye zamu yake?
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics