Katikati Ya Washtakiwa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Katikati ya washtakiwa, Waliosimama hukumuni
Nilikuwa mmoja wao, Hukumu ilisomwa kwetu
Sikuamini kusikia, Kwamba nimehukumiwa kifo
Faraja ingetoka wapi? Moyoni nikakata tamaa
Refrain
Nyuma yangu nikasikia, Sauti ikisema kwangu
Mkombozi yuko mlangoni, Kashuka toka juu
Ameshindwa kuvumilia, Kachukua nafasi yangu
Nimekuwa mtumwa huru, Hakika niko huru
2. Katikati ya washtakiwa, Waliotafutwa kwa bidii
Nilikuwa mmoja wao, Sababu nilimwacha Bwana
Nikatambua mbele yangu, Sina jinsi mimi ni wa kufa
Faraja ingetoka wapi? Moyoni nikasononeka.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics