Siku Ya Mwisho Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Siku ya mwisho tutakapoiona wingu angani (angani)
Yesu yuaja kutuchukua twende nyumbani (nyumbani)
Atupeleke mbinguni kwake Baba tupumzike (pumzike)
Yesu yuaja kutuchukua twende nyumbani (nyumbani)
Shida tulizoziona duniani tutasahau (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua Twende nyumbani (nyumbani)
2. Mwandame Bwana siku ya kuja kwake iko karibu (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua Twende nyumbani kwake
Makovu yote ya dhambi za dunia tutasahau (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua Twende nyumbani (nyumbani)
3. Rafiki zetu tulotengana nao tutawaona (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua Twende nyumbani kwake
Muda waisha jitayarishe sasa umwone Yesu (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua Twende nyumbani (nyumbani)
Ungali hai sahihisha mwenendo uokolewe (Yesu)
Yesu yuaja kutuchukua twende nyumbani kwake
4. Siku ya mwisho arejeapo Yesu tutasahau shida
Wote waliolala katika Bwana wataamshwa tena
Siku ya mwisho arejeapo Yesu tutasahau shida
Wote waliolala katika Bwana wataamshwa tena
Outro
Yesu; Yesu yuaja kutuchukua
Yesu; Yesu yuaja kutuchukua
Uwe tayari; Kuenda naye…
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics