Baba Tusamehe Lyrics sung by The Gospel Train

Baba Tusamehe Lyrics sung by The Gospel Train


Prelude

Baba tunakuja mbele zako leo, twakuomba ututakase


Verse 1/Prechorus

Baba tunanyenyekea, Twajikabidhi mkononi mwako

Mmmh Baba ["Baba - Baba"] sisi wenye dhambi ["Tunaomba mbele zako"]

Tunajitoa ututakase ["Tunajitoa - Tunaomba mbele zako - Ututakase"]


Oh Baba ["Baba-Baba"] tunanyenyekea,

Twajikabidhi mkononi mwako;

Wewe uliye wa mbinguni ["Yesu"]

Sisi wenye dhambi tunajitoa ututakase. ["Ututakase - Amen - Amen"]


Chorus 1a

Tumetenda maovu mengi ["Baba tusamehe"]

Tumetanga mbali nawe ["Sote twapotea"]

Tumeacha nuru ya kweli ["Tunarudi"]

Tunarudi leo Bwana ["Sisi wenye dhambi - Yesu"]

Tunarudi leo Bwana ["Ooh"]


Chorus 1b

Tumetenda maovu mengi ["Baba tusamehe"]

Tumetanga mbali nawe ["Tumetanga - Baba - Baba"]

Tumeacha nuru ya kweli ["Baba - Tuna..."]

Tunarudi leo Bwana ["Yesu - Tuna..."]

Tunarudi leo Bwana.



Verse 2a

Yesu alishuka chini ["Kwetu"]

Kutukomboa kutoka dhambini ["Ooh Yesu"]

Yesu ["Yesu - Yesu"] alisulubiwa ["Yesu alisubiwa"]

Ili mi' na we' tuokolewe ["Sikiliza"]


Verse 2b

Yesu ["wetu"] alishuka chini

Kutukomboa kutoka dhambini [Baba - Yesu - Yesu]

Yesu ["Yesu - Yesu"] alisulubiwa

Ili mi' na we' tuokolewe


Chorus 2a

Yesu ni tumaini letu ["Baba wa mbinguni"]

Yesu anatutakasa

Yesu ni mwanzo tena mwisho

Alfa na Omega ["Yesu kimbilio!"]

Yesu kimbilio letu ["Mwamba wa imara"]

Yesu kimbilio letu ["Oh, Yesu kwetu ni kimbilio!"]


Chorus 2b

Yesu ni tumaini letu ["Mwamba wa imara"]

Yesu anatutakasa ["Anatutakasa"]

Yesu ni mwanzo tena mwisho,

Alfa na Omega

Yesu kimbilio letu ["Baba wa mbinguni"]

Yesu kimbilio letu ["Tumetenda dhambi"]


Chorus 1a.2

[Ooh Tumetenda...]

Tumetenda maovu mengi ["Baba tusamehe"]

Tumetanga mbali nawe ["Tunarudi* Yesu tusamehe"]

Tumeacha nuru ya kweli ["Sisi wenye dhambi"]

Tunarudi leo Bwana ["Wetu - Tunarudi Baba* - Tunarudi leo"]

Tunarudi leo Bwana ["Baba tumetenda"]



Chorus 2b.2

Tumetenda maovu mengi ["Baba tusamehe"]

Tumetanga mbali nawe

Tumeacha nuru ya kweli ["Tumeacha nuru ya kweli, lakini leo Bwana tunarudi kwako - Ooh"]

Tunarudi leo Bwana [Tunarudi Bwana - Miaka mingi tumetanga lakini leo tunarudi Bwana"]

Tunarudi leo Bwana ["Mwamba wa imara"]

Tunarudi leo Bwana ["Makosa zetu tusamehe Baba"]

Tunarudi leo Bwana ["Utukumbuke katika ufalme wako - sisi wote"]

[Wetu] Tunarudi leo Bwana

Tunarudi leo Bwana...


The Gospel Train, Kenya.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Damu Yake Lyrics sung by The Golden Gate Choir

Nyosha Mkono Wako Lyrics sung by Nyandema SDA Choir