Kwanza Kapita (Tenda Wema) Lyrics sung by Messengers
1. Kwanza kapita yule mlawi, Kachungulia akatoweka
Kisha kapita yule kuhani, Kama yule mlawi akatoweka mbali
Bila huruma bila msaada, Kwa aliyepigwa njiani
Wakamwacha bila msaada, Moyo wa chuki wa ukatili
Refrain
Akapita msamaria, Akaonyesha huruma (Haleluya)
Akaonyesha upendo (Haleluya)
Akaguswa na hali yake
Mara ngapi ndugu yangu, Umeonyesha huruma
Kwa wale wenye mahitaji
Hebu uwe Msamaria mwema
2. Kila siku utende mema, Heri kwa watendao mema
Bila kuchoka toa msaada, Japo kidogo kwa jirani
Siku zote ondoa chuki, Sisi sote tu wana wa Mungu.
Messengers.
Messengers, Simba Wa Yuda Vol 3, Bedi Score, Bedi Lyrics