Tuesday, 5 May 2026

Nipe Biblia Lyrics sung by Light Vocal Band

Nipe Biblia Lyrics sung by Light Vocal Band

1. Nipe Biblia nyota ya furaha, Wapate nuru wasafirio

Hakuna la kuzuia amani, Kwani Yesu alituokoa

Refrain

Nipe Biblia neno takatifu, Nuru yake itaniongoza

Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea

2. Nipe Biblia nihuzunikapo, Ikinijaza moyoni dhambi

Nipe neno zuri la Bwana Yesu, Nimwone Yesu Mwokozi wangu

3. Nipe Biblia nipate kuona, Hatari zilizo duniani

Nuru ya neno lake Bwana Yesu, Itaangaza njia ya kweli

Refrain

Nipe Biblia neno takatifu, Nuru yake itaniongoza

Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea

4. Nipe Biblia taa ya Maisha, Mfariji tunapofiliwa

Unionyeshe taa ya mbinguni, Nione utukufu wa Bwana

Refrain

Nipe Biblia neno takatifu, Nuru yake itaniongoza

Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea

From: Nyimbo Za Kristo No. 052

Writer: Priscilla Jane Owens.

Light Vocal Band.

Light Vocal Band, Swahili Hymns, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...