Bwana Naomba Roho Wako Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Bwana naomba roho wako,
Aingie moyoni mwangu, Nami nikutukuze
Unionyeshe wema wako,
Unifundishe pendo lako, Nami nikutukuze.
Refrain
Bwana naomba unisikilize,
Ninahitaji unijaze na roho
Uwashe moto ndani yangu,
Watu wa dunia wajue, Kwamba wewe ni Bwana.
2. Kama wakati wa mitume,
Bwana uliwajaza roho, Na wakashuhudia
Na nguvu kutoka mbinguni,
Watu wengi waliokoka, Bwana ulitukuzwa.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Vol 27, Bedi Score, Bedi Lyrics